Jumamosi , 4th Feb , 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametoa maelekezo kuwa Serikali isimamie msiba wa watu 17 waliofariki kwa ajali mkoani Tanga hadi utakapomalizika.

Gari lililopata ajali

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba, ameyasema hayo kwamba serikali itagharamia msiba wa ajali hiyo ikiwa ni maelekezo ya Rais Samia kutokana na msiba huo ni wa Taifa hivyo serikali itaendelea kubeba gharama hizo.

Mgumba ameyasema hayo katika eneo la ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo Februari 4, 2023, wilayani Korogwe iliyohusisha Fuso iliyokuwa ikielekea Dar es Salaam na gari ya abiria aina ya Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu kutokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro na kusema watashirikiana na familia ili kujua utayari wao wa kusema kati ya leo au kesho

"Tunashirikiana na wanafamilia ili kujua utayari wao, wapo tayari kusafiri leo au kesho lakini kama serikali tutagharamia msiba huu kwa maelezo ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwa msiba huu ni wa Taifa, na serikali tutaendelea kubeba gharama hizi" amesema Mgumba.