Ijumaa , 25th Nov , 2022

Serikali Imesema haitamvumilia mtu,watendaji ama taasisi mbayo itakwamisha au kuchezea Mifumo ya serikali mtandao ikiitaka bodi ya serikali mtandao kuepuka rushwa katika utendaji kazi wake.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejiment ya utumishi wa umma utawala bora Jenister Mhagama

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejiment ya utumishi wa umma utawala bora Jenister Mhagama Mara baada ya kuzindua bodi ya serikali mtandao ambapo ameitaka bodi hiyo kuhakikisha mifumo ya taasisi zote inakamilishwa na kuwa na uwezo wa kubadilishana Taarifa.

Jenister amesema matarajio ya serikali ni kuona hata mwananchi mwenye simu ya tochi anapata huduma kupitia serikali mtandao kama ambavyo ilivyo kwenye malipo ya serikali Bill za maji na umeme kwa ghafama nafuu zaidi

Hata hivyo kupitia watalaam wa bodi hiyo iliyozinduliwa imesema changamoto ya mifumo ni kubwa na kuwatahadharisha wahalifu wenye nia ovu kuwa  watahakikisha kupitia serikali mtandao serikali Itafikia azma yake bila kuionea haya taasisi itakayokwamisha mifumo.

Bodi hiyo imezinduliwa rasmi hii Leo mara baada ya Rais Samia Suluhu kumteuwa Mwenyekiti wake Dkt Mussa Kisaka ambapo imesisitizwa kuwekeza katika teknolojia kwa kuwa mifumo inabadilika kila kukicha.