Serikali yaeleza matokeo ya ujenzi wa viwanda 100

Jumatano , 12th Jun , 2019

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwita Waitara, amesema mpaka sasa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wamewezesha ujenzi wa viwanda takribani 3000, tangu lilipotolewa agizo la ujenzi wa viwanda 100 katika kila Mkoa.

Naibu Waziri Waitara amebainisha hayo Bungeni jijini Dodoma wakati wa muendelezo wa maswali na majibu wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum (CHADEMA) Sophia Mwakagenda.

Mwakagenda ameuliza kuwa "suala la ujenzi wa viwanda 100 kila Mkoa lilitamkwa kisiasa, Serikali ituambie vimejengwa viwanda vimejengwa vingapi tangu agizo hilo litolewe."

Akijibu swali hilo Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waiata amesema kuwa "hili si tamko la kisiasa na linatekelezeka, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wameshaelekezwa, baadhi ya Halmashauri wameshatenga maeneo kwa ajili ya zoezi hili na mpaka sasa zaidi ya viwanda 3000 vimeshajengwa"