Jumatatu , 6th Mar , 2023

Chama kikuu cha siasa cha upinzani nchini Sudan Kusini, Sudan People's Liberation Movement in Opposition (SPLM-IO), kinamtaka Rais Salva Kiir kumrejesha madarakani Waziri wa Ulinzi Angelina Teny.

 

Rais Kiir alimfuta kazi Bi Teny siku ya Ijumaa . Alikuwa waziri wa kwanza mwanamke wa ulinzi nchini humo. Rais huyo pia alimfukuza waziri wa mambo ya ndani Mahmoud Solomon. Hakuna sababu zilizotolewa za kufukuzwa kwao.

Bw Kiir pia alibadilisha Wizara ya Ulinzi kwa chama chake cha kisiasa, Sudan People's Liberation Movement (SPLM) na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa SPLM-IO.

Chama cha upinzani cha SPLM-IO  kimelaani na kukata kuondolewa  kwa Bi Teny. Iliitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji wa makubaliano ya amani yaliyofufuliwa, ambayo yanavipa vyama mamlaka ya kuwaondoa wawakilishi wao katika baraza la mawaziri na kuteua watakaochukua nafasi hiyo kwa kumjulisha rais.

SPLM-IO   Ilisema kubadilishana kwa wizara hizo pia kunakiuka masharti ya makubaliano ya amani - ambayo yanahitaji pande husika kukubaliana juu ya ugawaji na uteuzi wa wizara katika serikali ya umoja wa kitaifa..

Katika taarifa, Riek Machar, kiongozi wa SPLM-IO na makamu wa kwanza wa rais, alitoa wito kwa rais kubatilisha amri ya upande mmoja, akiongeza kuwa chama chake kimejitolea kufufua makubaliano hayo.

Wachambuzi wanasema hatua ya hivi karibuni inaonekana kuashiria kuwa uhusiano kati ya Bw Kiir na Bw Machar bado umevurugika