Jumanne , 1st Sep , 2015

WAZIRI mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amesema kuwa mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) waziri wa zamani Edward Lowassa hakuwa na kosa wakati wa Richmond alijitoa kafara kwaajili ya nchi na ndio maana hakufukuzwa kazi.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye akiwana mgombea urais kupitia Chadema,Edward Lowassa

Sumaye ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa mkoa wa Njombe katika mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia UKAWA Mkoani Njombe alisema kuwa Lowassa hakuwa na kosa na ndio maana aliamua kujiondoa mwenyewe na kuwa ndio maana hakufukuzwa.

Amesema kuwa kama Lowassa alikuwa ana kosa angefukuzwa wakati uleule na angechukuliwa hatia kipindi kile na kuwa alijiondoa kwa kulinda heshima ya Rais.

Lowassa aliamua kujitoa kama kondoo wa Kafara hakuwa na kosa na kama wakija CCM wawaulize baada ya hapo walifanya nini na hawataweza kudhibiti rushwa kwa kuwa Escrow walishindwa.

Amesema kuwa wananchi hawata pata umeme vijijini cha zaidi wanapewa adhabu ya kupandishiwa mafuta kwa kuwaogopa matajili wenye vituo vya mafuta.