
Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa,
Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 20, 2022, Bungeni Dodoma, wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
"Nimshukuru Rais Samia kwa kutoa idhini ya ajira za watumishi wa afya na elimu 17,412, ambapo nafasi 9,800 ni za walimu na 7,612 ni kada za afya ambao wataajiriwa mwaka huu wa fedha 2021/22, nitoe taarifa rasmi kwamba Watanzania wenye sifa wanaelekezwa kuomba kuanzia leo, maombi ya ajira hizi ni bure," amesema Waziri Bashungwa.