
Mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila
Hayo ameyasema katika mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero zinazowazonga wananchi, uliofanyika Stendi ya zamani ya mabasi mjini Bariadi mkoani humo, ambapo amesema Tanzania pia inaongoza kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki kwa kufikisha umeme katika maeneo ya pembezoni.
Aidha, RC Kafulila akatumia nafasi hiyo kutoa siku 60 kwa taasisi za umma mkoani humo kuondoka kwenye majengo ya kupanga na kuelekea Nyaumata, ili kuiondolea serikali mzigo wa kodi.