Jumatatu , 16th Jun , 2014

Jumla ya watoto 963 wamelawitiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita nchini Tanzania, huku sababu kuu ikitajwa kuwa ni ukatili unaofanywa dhidi yao pamoja na ukosefu wa mfumo bora na unaoeleweka wa kuwalinda watoto dhidi ya hatari na majanga.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa kituo cha sheria na haki za binadamu, mwanasheria Harold Sungusia (kushoto).

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Bw. Harold Sungusia, amesema hayo leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kimataifa ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo amesema takwimu hizo ni wastani wa watoto wawili walikuwa wakilawitiwa kila siku.

Kwa mujibu wa Sungusia, wengi wa watoto hao, wamefanyiwa kitendo hicho cha kikatili na ndugu zao wa karibu, ambao wamepewa jukumu la kuwatunza ambapo kuna haja ya serikali kuhakikisha kuwa inaandaa mfumo utakaotoa ulinzi kwa watoto hasa kupitia sheria ya haki na ulinzi wa mtoto ya mwaka 2009.