Prof Tumaini Nagu ametoa rai hiyo wakati akizindua application maalum iliyoandaliwa na Taasisi ya Chakula na Lishe ambayo imelenga kutoa taarifa sahihi juu ya ulaji salama unaofaa ikianza na watu wanaishi na virusi vya ukimwi.
Pia ametoa maelekezo kwa taasisi ya chakula na lishe nchini kutazama maeneo ya mama wajawazito na watoto pia kwa wanawake waliofikia umri wa kuzaa sambamda na makundi ya wagonjwa ka figo,moyo kisukari kupata taarifa mapema kupitia mfumo huo.
Kwa upande wake Mganga mkuu mkoa wa Dar es Salaam Dkt Rashid Mfaume ameyataja maeneo kwa mkoa huo ikiwemo wilaya ya Temeke kuwa na changamoto ya lishe akitumaini mfumo huo kuja na majibu kwa wakazi hao huku hali ya mkoa kwa upande wa udumavu ikiwa 18 asilimia ambayo iko chini ya kiwango cha Shirika la Afya duniani WHO
Hata ivyo Mkurugenzi mtedaji wa taasisi ya chakula na lishe Dkt Germana Leyna amesema lengo la kuanzisha application hiyo ya mobile ni kuhakikisha elimu inawafikia watanzania wengi zaidi licha ya kuanza na watu wanaishi na virusi vya ukimwi.




