Wajumbe wa Tume ya Rais ya uchunguzi wa matukio ya vurugu yaliyofanyika wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29 Mwaka jana imefika Mkoani Mara kwa lengo la kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusiana na matukio yaliyotokea ikiwemo vifo.
Akizungumza wakati wa kuwapokea jopo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi, amelipongeza jopo hilo kwa kufika Mkoani humo na kuwataka kufanya kazi ya uhuru akiwahakikishia kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wananchi wa maeneo watakayo tembelea kwa ajili ya kukusanya maoni.
Waliofika Mkoani Mara kwa ajili ya kukusanya maoni hayo ni Balozi Radhia Msuya na Balozi David Kapya ambapo tayari wameelekea Wilayani Tarime kwa ajili ya kukusanya maoni kisha watafanya hivyo katika wilaya ya Bunda na Musoma.

