Jumatano , 20th Dec , 2017

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema hadi sasa hakuna chama chochote cha siasa kilicho fuata sheria na kanuni za uchaguzi za kujitoa katika uchaguzi wa marudio wa ugombea ubunge na udiwani na wabungeutakao fanyika Januari mwakani.

Akizungumza na vyombo vya habari Leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Tume hiyo Bwana Ramadhani Kailima amesema kuwa mgombea wa jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bwana David Joseph Njumbe amekidhi vigezo vya Kikatiba na Sheria za Uchaguzi na tayari amejaza fomu zote na kuzirejesha tume hiyo hivyo kauli za viongozi wa juu wa vyama vya siasa kumkataa mgombea wao sio kazi ya tume hiyo bali na masuala ya vyama vyenyewe.

Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema suala la vyama kujitoa katika uchaguzi ni jambo la kawaida na limekuwapo tangu chaguzi za mwanzo nchini na kuvikumbusha vyama vya siasa kufuata taratibu na kanuni za kuwasilisha malalamiko yao.

Mbali na hayo Bw. Kailim ameongeza kwamba wao wanatambua vyama vyote vya siasa vitashiriki uchaguzi huo.