Jumanne , 14th Feb , 2023

Tume ya Tehema Tanzania yasaini mkataba na UNESCO (ICTC) imesaini mkataba wa ushirikiano na UNESCO kwa ajili ya utafiti wa matumizi ya intaneti. 

Mkurugenzi wa Tume hiyo Nkundwe Moses Mwasaga (Kushoto) na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNESCO Tanzaniae Michael Toto

Mkurugenzi wa Tume hiyo Nkundwe Moses Mwasaga, amehakikisha kuwa utafiti unaoenda kufanyika unaweza kusaidia katika utekelezaji wa sera za kitaifa katika mapinduzi ya TEHAMA.

"Kiukweli utafiti kama huu kwa nchi yetu ulitakiwa kufanyika muda mrefu sana kwani masuala ya intaneti hayajaanza leo Tanzania," amesema Mwasaga

Mwasaga amebainisha kuwa Tume ya TEHAMA ndio inasimamia sera ya taifa kwenye TEHAMA na utafiti huu utaisaidia Tume katika utekelezaji wa kazi zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNESCO Tanzaniae Michael Toto amesema ICTC na UNESCO zinasaini mkataba huo kwa ajili ya ushirikiano wa utafiti kuangalia maendeleo na matumizi ya intaneti Tanzania na kwamba ni mwitikio wa wito wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo mwaka jana alipowasili makao makuu ya UNESCO Paris Ufaransa aliwasihi kuendelea kutoa ushirikiano katika kujenga jamii yenye usawa na uelewa wa masuala mbalimbali ya teknolojia.

Utafiti huo utanazamiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu na baada ya hapo matokeo ya utafiti yatatumika katika utekelezaji wa sera mbalimbali za masuala ya teknolojia nchini.