
Takribani vijana zaidi ya elfu sabini na saba katika jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma hawana ajira zakuwaingia kipato.
Akizungumza na East Africa Radio Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Injinia Atashasta Nditie amesema tatizo lakuwepo kwa vijana wengi ambao hawana ajira nikutokana na asilimia kubwa ya vijana wamekuwa na imani potofu ya kutaka kuajiriwa na sio kujiajiri wenyewe.
Ameiomba serikali kuanzisha vyuo mbalimbali vya majaribio ya ufundi ambavyo vitawawezesha vijana wengi kujifunza na kwenda kujiajiri wenyewe na gharama ya vyuo hivyo vizingatie kipato cha watanzania wa hali ya chini.
Amesema kama vyuo hivyo vitaanzishwa vitaweza kuleta ajira kwa vijana walio wengi nchini na kuepusha vitendo mbalimbali vya kihalifu ambavyo vinaweza kufanywa na baadhi ya vijana ambao wako mitaani bila kazi zakufanya.
Kwa upande wa usalama katika mpaka karibu na nchi ya Burundi kwenye kambi ya Nduta jimboni humo ameiyomba serikali kuongeza usalama katika kambi hiyo, kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wakimbizi wasio waaminifu wanaofanya vitendo vya uhalifu katika maeneo jirani na kambi hiyo sambamba na kuongeza vifaa vya ulinzi na usalama.

