
Mratibu wa kitaifa wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC Onesmo ole Ngurumwa
Akitoa taarifa hizo mratibu wa kitaifa wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC Onesmo ole Ngurumwa ametoa wito huo katika kikao cha kuhakiki mpango kazi wa kitaifa wa haki za binadamu na asasi za kiraia.
Awali mgeni rasmi wa mkutano huo Dkt Khatibu Malimi Naibu katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria amesema ili kukamilisha mpango huo zipo taratibu na awamu za kupitia ikiwemo uandaaji utekelezaji, Ufuatiliaji pamoja na ukusanyaji maoni na mapendekezo ya wananchi na wadau wa haki hivyo kuwataka wadau kushiriki katika kutoa maoni Ili kukamilisha Mpango huo wa pili.
Hata hivyo upande wao washiriki na wadau wa haki wamesema kupitia maoni ya wadau wanatarajia kukamilika kwa Mpango huo.