Jumanne , 15th Feb , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limekamata mtandao wa watu tisa (9) ambao wametajwa kuhusika na tuhuma za mauaji pamoja na kuendesha biashara ya mauziano ya viungo mbalimbali vya sehemu ya mwili wa binadamu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, amesema mtandao huo umekamtwa ikiwa ni siku chache tu baada ya kutokea mauaji ya kinyama ya binti mmoja uko wilayani Sikonge mkoani humo ambaye aliuawa na kutolewa sehemu za siri.

Amesema kufuatia tukio hilo la mauaji jeshi la polisi lilianza kwa kukamata watu watatu baada ya kuwatilia mashaka ambapo walimtaja mganga wa kienyeji ambaye amekuwa akinunua viungo vya mwili ikiwemo sehemu za siri za jinsia zote pamoja na matiti.