Alhamisi , 2nd Oct , 2025

Baada ya teuzi hizo viongozi viongozi hao wanatarajiwa kuanza majukumu yao mara moja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali leo Oktoba 2, 2025.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Dkt. Samia amemteua Bw. Said Habibu Tunda kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) akichukua nafasi ya Dkt. Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Aidha, rais Samia amemteua Bw. Pius Andrew Ng’ingo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kamuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) akichukua nafasi ya Bw. Waziri Kindamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa pia.

Baada ya teuzi hizo viongozi viongozi hao wanatarajiwa kuanza majukumu yao mara moja.