Alhamisi , 30th Dec , 2021

Shule ya Msingi Mkapa iliyopo Mpanda mkoani Katavi, inakabiliwa na upungufu wa madarasa na kuelemewa na idadi kubwa ya wanafunzi hali inayopelekea wanafunzi zaidi ya 250 kukaa darasa moja tena chini ili waweze kutosha hali inayopelekea walimu washindwe hata kusogeza miguu yao.

Sehemu ya majengo ya shule ya msingi Mkapa

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa shule hiyo Didas Ngua, wakati akitoa taarifa kwa mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya jimbo lake.

Kwa upande wao walimu wa shule hiyo wemeeleza adha wanayokumbana nayo wakati wa ufundishaji na zaidi ni usikivu mdogo kwa wanafunzi unaosababishwa na mazingira yasiyo rafiki kwa ujifunzaji na kwamba kutokana na idadi ya wanafunzi kuwa kubwa darasani inapelekea wakati mwingine kusogeza miguu ya wanafunzi hao ili na wao wapate sehemu ya kukanyaga.