Jumanne , 25th Jan , 2022

Wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kododo Tarafa ya Mgeta wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wapo katika hatari ya kuangukiwa na madarasa wanayoyatumia kufuatia madarasa hayo ambayo yamejengwa kwa mawe tangu mwaka 1970 kuanza kupasuka kisha kudondosha mawe.

Wanafunzi wakiingia katika moja ya madarasa

Haya yamebainika mara baada ya East Africa TV kufika katika eneo hilo na kushuhudia uchakavu wa madarasa ya shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya mia saba, ambapo wanafunzi wanaosma katika shule hiyo wameiomba serikali kuwajengea madarasa mapya.

Kutokana na hali hiyo madiwani wa kata tatu zilizopo Tarafa ya Mgeta, wamesema kuwa hali hiyo haikubaliki na wamewataka wananchi wa kijiji cha Kododo kuhakikisha wanaanza nguvu ya kuanza ujenzi wa madarasa mapya.