
Law School
Akizungumza na East Africa TV & Radio digital, hii leo Aprili 25, 2023, Afisa habari wa taasisi hiyo amesema matokeo haya ya mtihani yametolewa wiki iliyopita na hawa ni wale wanafunzi waliojiunga na Law School januari 2022.
Ikumbukwe ripoti iliyotolewa na Dkt Harrison Mwakyembe, kufuatia kamati iliyoundwa mwaka 2022 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro, kuhusu ubovu wa matokeo katika taasisi hiyo, ripoti ilitaja kuwa uwezo mdogo wa wanafunzi wengi wanaoruhusiwa kusoma sheria na baadae kujiunga na taasisi katika kumudu lugha ya kufundishia ya kiingereza.
Na kwamba hilo ni moja ya tatizo lenye athari kubwa katika uelewa wa amsomo na kujieleza.