Jumatatu , 27th Mar , 2023

Kundi la wanamgambo wa Codeco siku ya Jumapili liliwaua watu 17 iliowakamata katika eneo la Djugu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 

 

Waathiriwa walikuwa abiria waliokuwa ndani ya magari manne yaliyokuwa yakielekea Mungwalu, katika mkoa wa Ituri, Redio Okapi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti.

Walitekwa nyara baada ya wanachama watatu wa Codeco kuuawa katika makabiliano na wanamgambo hasimu, redio hiyo iliongeza.

Miongoni mwa waliotekwa nyara ni mwanamke mjamzito, Mamlaka za eneo hilo bado hazijatoa tamko lolote kuhusiana na shambulio hilo.

Codeco, wanamgambo wanaodai kulinda jamii ya wakulima wa Lendu huko Ituri, ni mojawapo ya makundi yenye silaha yanayoendesha shughuli zao katika eneo hilo lenye utajiri wa madini.