
RC Mongella ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Arusha, amewataka wote wanaopotosha kwa makusudi zoezi la uwekaji alama katika eneo hilo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 1,500 ambalo ni eneo linalopaswa kuhifadhiwa, kuacha kufanya hivyo kwa kuwa lengo la serikali ni kuhifadhi eneo hilo kwa manufaa ya Watanzania na uchumi wa nchi kwa ujumla wake.
Akizungumza katika kikao kazi kuhusu maendeleo ya uhifadhi wa Pori Tengefu la Loliondo, wilayani Karatu, Arusha, Mongella amesema pia kuwa maandalizi ya kuhamisha wananchi kwa hiyari katika eneo la Ngorongoro kuelekea Handeni, Tanga yanaendelea vizuri yote yakiwa na lengo moja la kuhakikisha uhifadhi endelevu katika Hifadhi ya Ngorongoro.
“Ameeleza kuna baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha umma zoezi hili na kuhusishwa na watu kuhama ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kitu ambacho sio kweli”