Ijumaa , 12th Aug , 2022

Wanawake nane wameuawa kwa nyakati tofauti katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kwa kipindi cha kuanzia Machi hadi Agosti mwaka huu, akiwamo mwalimu wa shule ya msingi Mbanju ambaye aliuawa kwa kupigwa mawe, huku mapenzi na ugomvi wa mali ukitajwa kama chanzo cha mauaji hayo.

Mawe

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara ACP Nicodemus Katembo, amesema mauaji ya watu watano kati ya nane yanahusishwa na wivu wa mapenzi, huku mauaji ya watu wawili yakihusishwa na kuwania mali, na tukio moja ni mtuhumiwa kumuua ndugu yake kutokana na kuwa na ugonjwa wa akili.

Aidha ACP katembo, amesema tayari watuhumiwa wa mauaji hayo wameshakamatwa na wengine wamefikishwa mahakamani