Alhamisi , 4th Aug , 2016

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mhe. Seleman Jaffo, ametoa wito kwa wataalamu wa Mazingira kusimamia vyema mradi wa ujenzi wa madampo ya kisasa na uboreshaji wa usafi katika Majiji saba nchini ili kuondoa kero ya uchafu.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mhe. Seleman Jaffo.

Naibu Waziri Jaffo ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati akikabidhi mitambo ya Usafi na ujenzi wa madampo pamoja na kufungua semina ya siku saba ya wataalamu wa mazingira na usafirishaji kutoka majiji Saba nchini Tanzania.

Mhe Jaffo ameuzungumzia mradi huo unaotekelezwa n wizara yake kwa ufadhili wa Benki ya Dunia pamoja na miradi mingine isimamiwe vyema huku akionyesha kutoridhishwa na ujenzi wa stand ya Korogwe mkoani Tanga ambayo imegharimu mamilioni ya shilingi.

Aidha Mhe Jaffo amewataka watendaji wa na watalaamu wa Jiji la Arusha kwa kuwa ndio kitovu cha Utalii nchini hivyo madhari ya jiji hilo yatazidi kuvutia zaidi watalii kuja nchini.

Pia Naibu Waziri huyo amewata wataalamu hao mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo watumie ujuzi wao kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya kuuweka mji huo safi kwa kuwa ndio yatakuwa makao makuu ya serikali.

Sauti ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mhe. Seleman Jaffo, a