Ijumaa , 27th Jun , 2014

Watu watatu wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah kupasuka tairi ya nyuma na kupinduka mara tatu katika kijiji cha Januka manispaa ya Singida.

Gari iliyopata ajali

Watu watatu wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah kupasuka tairi ya nyuma na kubingirita mara tatu katika kijiji cha Januka manispaa ya Singida.

Akithibitisha kitokea kwa vifo hivyo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktari Deogratias Banuba amesema wamepokea maiti mbili wakiwa wamesha fariki eneo la tukio akiwemo dereva wa Noah Enock Mbaga, binti Ajira Juma na maiti nyingine ya Bi Tatu Bunku ambaye alikuwa mkuu wa shule ya sekondari Ngimu amefia katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Daktari Banubasi amesema majeruhi kumi wamepatiwa huduma ya kushonwa sehemu mbalimbali za miili yao na wanaendelea na matibabu, pia hakuna majeruhi ambaye atapatiwa rufaa .

Mmoja wa majeruhi akiongea kwa shida huku akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida bwana Ramadhani Mlenga amesema gari lilikuwa katika mwendo wa kasi na gafla likaacha njia na kupinduka mara tatu.