Alhamisi , 24th Dec , 2015

Jumla ya watoto 12 wamezaliwa usiku wa kuamkia leo sikukuu ya Maulidi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Jumla ya watoto 12 wamezaliwa usiku wa kuamkia leo sikukuu ya Maulid katika hospitali ya taifa ya Muhimbili huku wakina mama waliojifugua watoto hao wakitoa pongezi kwa huduma bora waliyopata katika hospitali hiyo.

Akizungumza na East Africa Radio leo kiongozi mkuu wa Jengo la Wodi ya Watoto ambae pia ni afisa muuguzi mwandamizi Celestina Chambo amesema kuwa kati ya watoto hao wa kiume ni 9 na wa kike ni wa 3 huku wawili wakiwa ni mapacha na hali zao pamoja na mama zao zinaendelea vizuri.

Wakizungumza baada ya kujifungua Mariam Twaibu na Amina Said waliojifungua watoto wa kiume kila mmoja wamesema kuwa walipata huduma nzuri wakati wote wa kujifunguwa na kuwaasa wazazi kuwa na kauli nzuri kwa waaguzi kwani waaguzi huzidiwa na idadi kubwa ya wazazi.