Jumamosi , 30th Jan , 2016

Watu hao walikwama kwenye mgodi baada ya kutokea maporomoko katika machimbo ya madini ya gypsum katika mkoa wa Shandong Mashariki mwa china tarehe 25 Desemba 2015.

Katika mgodi huo wachimbaji madini 29 walikwama baada ya maporomoko kati yao15 kufikia sasa wameokolewa wakiwa hai na mmoja amethibitika kupoteza maisha.

Wachimbaji hao wanne waligunduliwa wakiwa umbali mita 200 chini ya ardhi na operesheni ya kuwaokoa ilikamilika huku wangine 13 wakiwa hawajulikani waliko.

Watu 400 wameshiriki katika oparesheni ya kuwaokoa watu hao, na waliopatikana wanaendelea na matibabu hospitalini.

Aidha nchini Tanzania eneo la Nyangalata Novemba 2015 walikwama wachimbaji wadogo 5 mgodini kwa siku 41 na kuokolewa wakiwa hai baada ya kuishi kwa kula vyura, mende na magome ya miti.

Chanzo BBC