Akisoma kesi hiyo namba 11 ya mwaka 2023 akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Felician Kapama, mwendesha mashtaka upande wa Jamhuri mkaguzi msaidizi wa polisi Ryoba Mkambala amesema kuwa kwa pamoja washtakiwa hao walishiriki kumuua mtu huyo
Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo
Hakimu Felician ameiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 18 April kesi hiyo itakapotajwa tena, huku washtakiwa wakirudishwa rumande kwakuwa kesi hiyo haina dhamana.



