
Dkt. Kigwangala ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Temeke, kujionea utendaji wa wafanyakazi wa hospitali hiyo.
Aidha, Dkt. Kigwangala amesema hatua hiyo anaichukua kwa makusudi ili kuwa fundisho kwa wauguzi wote nchini ambao wamekuwa wakiikwamisha serikali katika jitihada za kukabiliana na vifo vya wakina mama wajawazito na watoto.