Barabara Sudan Kusini zimekua mbovu sababu ya mvua kubwa zinazoendela kunyesha ambazo zimesababisha njia kutopitika sababu ya mafuriko na matope.
Zaidi ya malori 1,500 yaliyobeba vyakula na mahitaji ya msingi yamekwama huko Magharibi mwa nchi hiyo.
Waziri huyo amesema kwamba wakandarasi wanafanyia kazi suala hilo ikiwemo kuharakisha malori kufika eneo la wahitaji
Barabara za Sudan Kusini zinatajwa kwamba ni mbovu kwenye ukanda wa Afrika kwa mujibu wa ripoti i liyotolewa na Bodi ya mamlaka ya usafiri Mashariki na Kaskazini mwa Afrika (NCTTCA).