
Waziri Mhagama ametoa agizo hilo leo katika mkutano wa pamoja baina ya serikali na vyama vya wafanyakazi, ambapo amevisisitiza vyama hivyo kuondoa kero hususani zile zinazohusiana na maslahi ya kazi.
Mkutano huo umeitishwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA, ambapo Rais wa Shirikisho hilo Bw. Tumaini Nyamhokya ameiomba serikali kutovichukulia vyama hivyo kama maadui.
Nyamhokya pia ameiomba serikali kuyasikiliza na kuyafanyia kazi madai ya wafanyakazi yanayowasilishwa na shirikisho hilo kwani hilo ndilo jukumu la vyama vya wafanyakazi mahali popote pale.