Ijumaa , 13th Dec , 2019

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kumshusha cheo kimoja Kamanda wa Polisi wa Kusini Pemba, Hassan Nassir Ali.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni

Kwa mujibu wa Mhandisi Masauni amemuagiza pia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, kuwaondoa ma RPC wote  wawili kisiwani Pemba kwa makosa ya kushindwa kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 16 za makazi ya Polisi, uliozinduliwa mwishoni mwa mwaka 2018 pamoja na kucha mikutano ya siasa ya chama cha ACT Wazalendo, kuendelea kufanyika kisiwani humo ikiwa ni kukaidi agizo la Mkuu wa Nchi.

"Namuagiza IGP awaondoe ma RPC wote Pemba na sio kuwapeleka wakawe ma RPC Mikoa mingine, maana majukumu hayo yamewashinda, pia namuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amshushe cheo kimoja yule RPC wa Kusini Pemba Hassan Nassir, yeye najua hana uwezo huo sababu si mamlaka yake, lakini mchakato wa mapendekezo unaanzia kwake kwahiyo aanzishe mchakato wa mapendekezo" amesema Mhandisi Masauni.