
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara, akila kiapo cha utii mbele ya Rais Dkt. Magufuli.
Waitara ambaye ameapishwa jana, Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kuteuliwa juzi Jumamosi, ambapo katika mazungumzo yake na www.eatv.tv, amesema kuwa hatokubali watu wamkwamishe katika utendaji kazi wake.
“Awe mpinzani au mtu yeyote sitokubali anikwamishe na nitashirikiana na kila mtu na namshukuru Mungu kwa nafasi hii na nitaitumikia kwa moyo wangu wote", amesema Waitara.
Akizungumzia kuhusu kuteuliwa kwake amesema kuwa, "Sikutarajia kama nitateuliwa kwa sababu sikujua kama Rais John Magufuli atafanya mabadiliko madogo katika mabaraza lake la mawaziri".
Waitara ambaye ni Mbunge wa Ukonga aliyejizulu ubunge akiwa CHADEMA na kuhamia CCM alipoteuliwa kugombea na kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi uliofanyikia Septemba 17, 2018 na kuibuka na ushindi kwa mara nyingine.