Ijumaa , 18th Nov , 2022

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani  Ramadhani Ng'anzi ametoa masaa 24 kwa wamiliki wa magari waliyoweka ving'ora na vimulimuli na hawatambuliki kisheria kuviondoa haraka iwezekanavyo

Ameagiza Wakuu Vikosi vya Usalama Barabarani kote nchini kuwakamata watakaokaidi agizo hilo kwa kuwapiga faini na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria

Kamanda Ng'anzi ametoa agizo hilo leo Jijini Dodoma kwenye zoezi la kujaribu vifaa na mfumo wa TEHAMA wa kudhibiti mwendo kasi ambapo amesema ving'ora hivyo vinatumika vibaya ile hali sheria imeeleza makundi ya kuvitumia na sababu zake,huku akitoa Siku 7 kwa Bodaboda kote nchini pamoja na abiria kuvaa kofia ngumu na agizo lifwatwe bila shuruti ya aina yoyote.