Ijumaa , 7th Oct , 2016

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kutuma timu ya wataalam kutoka Idara ya magonjwa ya mlipuko mkoani Kagera ili kwenda kushirikiana na timu ya mkoa ili kufanya tathmini ya magonjwa ya mlipuko.

Waziri Ummy Mwalimu akikabidhi misaada kwa mkuu wa mkoa wa Kagera

Hatua hiyo inakuja hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha mkoani humo.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu wakati akikabidhi misaada ya Dawa, Vifaa kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko mkoani humo.

Akizungumza baada ya kupokea misaada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu amewaomba wadau wengine kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya kurejesha hali ya kawaida baada ya maafa kutokea.