Jumanne , 20th Mei , 2014

Aliyekuwa msanii na muongoza filamu maarufu, Adam Kuambiana amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, katika mazishi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa mashabiki.

Jeneza la Marehemu Adam Kuambiana katika viwanja vya Leaders Club wakati wa shughuli ya kumtolea heshima za mwisho.

Maziko ya msanii huyu yameongozwa na viongozi mbalimbali akiwepo Waziri Wa Habari Vinana Tamaduni na Michezo Dr Fenella Mukangara, Mstahiki Meya wa Wilaya ya Kinondoni

Maziko ya masanii huyu ambaye umaarufu wake mkubwa umetokana na ushiriki katika filamu kama vile Fake Pastors, Fake Sons, na Regina, yametanguliwa na shughuli ya utoaji heshima za mwisho kwa mwili marehemu iliyofanyika katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.

Wakitoa maneno yao ya mwisho kwa Marehemu na kwa waliohudhuria msiba huu, kwa niaba ya wengine Mheshimiwa Waziri amewataka wasanii kuendeleza moyo wa Marehemu Adam katika kuendeleza wasanii kimasomo.

Marehemu ameelezwa kupoteza maisha kutokana na tatizo la Vidonda vya Tumbo.

Vilevile JB, Jokate, Mtunis kati ya wengine hapa wanaeleza namna Adam alivyokuwa mtu wa kipekee kwao, wakimpa sifa ya Muongoza filamu namba moja Tanzania.

Sauti ya Mheshimiwa Waziri Dr Fenella Mukangara akizungumza katika msiba leo
Sauti ya JB akizungumza na eNewz leo katika msiba
Sauti ya Jokate akizungumza na eNewz leo katika msiba