Alikiba azindua Unfogettable Tour, kuja na mambo 3

Ijumaa , 8th Nov , 2019

Msanii nguli wa Bongo Fleva, Alikiba amezindua rasmi tour yake ya 'Unfogettable' ambayo ameifanya kuwa maalumu kama zawadi ya miaka yake 17 katika muziki nchini.

Alikiba

Alikiba amesema hayo katika mkutano wake na wanahabari, uliofanyika katika hoteli ya Ramada Encore Posta Mpya, ambapo amethibitisha kuwa tamasha hilo litakuwa na mambo mengine mengi tofauti na muziki pekee.

"Kwa jinsi ambavyo mashabiki wangu wamenionesha upendo kwa miaka 17, nimeamua kuwaletea #AlikibaUnforgettableTour ambayo itakuwa na mambo mengi sana haiishii tu kuwa Concert au Tour", amesema Alikiba.
 
"#AlikibaUnforgettableTour itakuwa na mambo makubwa matatu. 1. Ujenzi wa #Ndotokazi kwa vijana, ambapo mimi na wenzangu watakaonishika mkono tutapita mikoani kuzungumza na wanafunzi wa vyuo. Jambo namba 2 kwenye #AlikibaUnforgettableTour ni #MedicalCamp, hapa namshukuru Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na jopo la madaktari, ambao watatoa mchango wa dawa kwa lengo la kutoa huduma ya afya kwa watu mbalimbali bure kabisa.", ameongeza. 

Aidha Alikiba amezungumzia jambo la tatu kuwa ni #FriendlyRegionalMatch ambapo yeye na watu wake watacheza katika kila eneo ambalo watakwenda, kwakuwa anapenda sana mpira na lengo lake kubwa ni kufanikisha hilo.

Alikiba amezishukuru East Africa TV na East Africa Radio kwa kuwa 'media partner' ambayo itazunguka katika kila mkoa atakaokwenda, "nitashirikiana na East Africa Television na East Africa Radio na nawashukuru sana", ameongeza Alikiba.