Jumanne , 4th Oct , 2022

Meneja wa msanii Sarahina Tz (Phina) D Fighter amesema kuna ugumu kwa msanii kupata Visa ya kusafiria kama hujasajiliwa na kutambuliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Picha ya Meneja D Figther na msanii wake Phina Tz

Akizungumza mbele ya Planet ya East Africa Radio Meneja D Fighter amesema "Mara nyingi ugumu unakuja kama msanii hajajisajili BASATA, inabidi Baraza likutambue kama msanii na iwe rahisi kutoa barua kufika katika balozi ya hiyo nchi".

Meneja D Fighter amesema hayo baada ya taarifa ya Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Babu Tale kujitolea kupambania Visa za wasanii wa Bongo kusafiri kuwania tuzo za AFRIMMA 2022.