Billnass ashindwa kujizuia kwa Nandy

Ijumaa , 14th Feb , 2020

Kila ifikapo Februari 14 ya kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya wapendanao maarufu kwa jina la Valentine Day, ambapo watu hutumia siku hii kama kuzidisha upendo na thamani kwa wapenzi wao.

Picha ya Billnass kushoto, kulia ni Nandy na rafiki yake akiwa na sare za mwanafunzi

Moja ya njia hizo ambazo watu wanafanya kwa wapenzi wao katika siku hii ni vitendo zaidi kama kupeana zawadi, kupiga picha za kumbukumbu, kwenda matembezi na mwenza wako au kupostiana katika mitandao ya kijamii ili kuzidisha upendo zaidi kwao.

Kwa upande wa msaniii Billnass yeye ameonesha kunogesha mahaba kwa kupost picha ya zamani ya Nandy akiwa na mavazi ya sare za mwanafunzi, halafu akaandika neno la Kiingereza, ambalo kwa lugha ya kiswahili linasomeka kama "isiyo na thamani", kisha akaweka alama ya kopa.

Inasemakana wawili hao wamerudiana tena baada ya siku za hivi karibuni, kuonekana wakiwa pamoja usiku na kupostiana katika mitandao ya kijamii hasa wa Instagram, hali ambayo inawapa maswali mengi mashabiki zao japokuwa wao wamekuwa wanakana kwamba hawapo kwenye mahusiano.