Calisah na Wema Sepetu tena, "hawezi kunikataa"

Jumatano , 20th Mei , 2020

Mwanamitindo Calisah amesema Wema Sepetu ni mmoja ya wapenzi wake ambao wanawasiliana sana na hata akitaka kwenda kwake hawezi kumkataza.

Mwanamitindo Calisah na staa wa filamu Bongo Wema Sepetu

 

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Calisah amesema  "Wema ndiyo mtu ninaye wasiliana naye sana, haipiti siku mbili kama hatujaongea na hapa kuna meseji zake sijui nikuonyeshe ila nitaonekana nam-snitch kwa sababu vitaleta miyayusho na siwezi kuonyesha kila kitu ila hatuna matatizo yoyote".

Aidha ameendelea kusema "Tupo na ukaribu ila sio wa mapenzi, sasa hivi ana wanaume zake anaendelea nao na mimi nina wanawake wangu, japo tunaonana na tunaongea hata nikitaka kwenda kwake na najua hawezi kunikataa".

Mahojiano kamili tazama kwenye video hapa chini