Jumatatu , 28th Oct , 2019

Msanii chipukizi wa filamu nchini aitwaye Serinza, amesema alikuwa anamtamani kimapenzi Irene Uwoya, alipokuwa anaongea nae kwenye simu huku akiwa kwenye jakuzi wakati wanaigiza filamu yao ya "tah tah".

Serinza ameiambia EATV & EA Radio Digital, kuwa kipindi cha nyuma kabla ya kuigiza filamu moja na mrembo huyo, alikuwa anatamani mwanamke mwenye muonekano kama wa Uwoya.

"Kabla ya kufanya kazi na Irene Uwoya, nilikuwa natamani kuwa na mwanamke kama Irene Uwoya, hisia zilikuwepo tangu tunarekodi  hizo audio halafu tukaenda kwenye video, ila siwezi kuelezea kitu gani ambacho kilikuwa kinatokea pale kwenye jakuzi hata mimi mwenyewe nilisikia tah tah na hata ule utamu ulikuwa mulemule ndani " ameeleza Serinza.

Aidha Serinza amemkandia Dogo Janja, ambapo amesema hadhani kama aliipata tah tah ya Irene Uwoya kwa sababu alikuwa hana maajabu.

"Sidhani kama Dogo Janja alikuwa ameipata ile tah tah ya ndani nadhani hajaifikia, kama alikuwa mumewe mbona sasa hivi sio mkewe, kuna wakati wa kulima na kupanda, yeye kwake ulikuwa wakati wa kulima sasa hivi wenzake tunapandana, nahisi ukiwa na maajabu kwa mtu fulani unaweza ukawa hadi mwisho labda hakuwa na yale maajabu" ameongeza.