Dogo Janja afichua uhusiano wake na Nandy

Jumatano , 15th Mei , 2019

Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ amefichua siri yake na msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ kwa kusema kuwa akiwa naye popote pale familia yake huwa na amani.

Dogo Janja akiwa na Nandy.

Dogo Janja amesema kuwa, alijuana na Nandy kabla hata hajaanza muziki na urafiki wao umefika hadi kwenye familia zao.

Ujue damu zetu zinaendana sana na ni mtu ambaye hata familia zetu zinafahamiana. Leo Nandy atakuja kwetu na mimi hivyohivyo kwao kwa hiyo hata nikiwa naye popote familia yake inakuwa na amani kabisa", amesema Dogo Janja.

Akizungumzia uhusiano wake na msanii mwenzake 'Billnas' ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na Nandy kipindi cha nyuma, Janjaro amesema kuwa yeye na Billnas wako vizuri na hajawahi kuwa na wivu dhidi yake.