Jumanne , 8th Sep , 2015

Mshindi wa milioni 1 wa mwezi Agosti, katika shindano la Fantasy League linalochezeshwa na East Africa Radio, Fredy Joseph Komba amesema ameshinda mkwanja huo kwa kuwa alikuwa akifahamu wachezaji wengi wanaocheza soka Uingereza na Hispania.

Mshindi wa milioni 1, Fredy Joseph Komba katika shindano la Fantasy League linalochezeshwa na East Africa Radio,

Fredy ambaye anatokea Mtwara amesema anaishukuru East Radio kwa kuanzisha shindano hilo, siri kubwa ya ushindi wake ikiwa ni kuchagua wachezaji wa timu ndogo ambao wana uwezo wa kukamia mchezo na kuibuka na ushindi wanapocheza na timu kubwa.

Mshindi huyo alifika studio za East Africa Television Mikocheni jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo na kukabidhiwa milioni moja yake.