Jumapili , 4th Jul , 2021

Imemchukua takribani siku 115 tu kwa Rapper na mwimbaji G Nako kutoka kundi la Weusi mpaka kutangaza jina la Extended Play (EP) yake mpya “Kiti Moto” ambayo anatarajia kuachia siku za hivi karibuni.

Picha ya Msanii G Nako

G Kankara aliipa muda wa miezi mitatu na siku 16 album yao “Air Weusi” wa kui-push sokoni kabla ya kuweka wazi ujio wake wa EP kupitia ukurasa wake wa instagram ambayo ilitoka Machi 12 mwaka huu ikiwa na nyimbo 14.