Gnako akataa kumuiga Nikki Wa Pili

Alhamisi , 5th Sep , 2019

EATV & EA Radio Digital  imepiga stori na msanii Gnako Warawara, ambaye amefunguka suala la familia yake , mavazi na 'issue' ya kumuiga Nikki Wa Pili kwa kumpost mpenzi wake.

Gnako na Nikki wa Pili wakiwa na wapenzi wao.

"Sio lazima kumuiga ni namna tu mtu anavyoamua kufanya mambo yake, pia ni aina ya maisha sidhani kama ni kitu ambacho natakiwa kukiiga au kukifuata kwa sababu mtu fulani anafanya", ameeleza.

Aidha Gnako amesema mwanaye wa kike anapenda sana kuimba na kuogelea ila atamuacha mwenyewe achague anachopenda kufanya kisha atampa muongozo.

Pia msanii huyo ameeleza kuwa anapenda sana mitindo na huwa anavaa kwa kuangalia mahali husika anapokwenda na hajawahi kujutia akiwa ametoka kwa kuona kama amevaa vibaya.

Gnako amejaliwa kupata watoto wawili na kwa sasa yupo nchini China na msanii Jux kwa shughuli zao binafsi.