
Grace Mugabe alimpiga binti aliyejulikana kwa jina la Gabriella Engels (20) ambaye ni mwanamitindo na kamba ya 'cable', baada ya kumkuta hotelini na watoto wake wa kiume Robert Mugabe Jr (25) na Chatunga Mugabe( 21)
Waziri wa Jeshi la Polisi wa Afrika Kusini aliviambia vyombo vya habari kuwa anatarajia kupokea ripoti rasmi ya uchunguzi wa tukio hilo, na ndipo sheria ifuate.
Vyombo vya habari kutoka Afrika Kusini vimeripoti kuwa Bi. Grace Mugabe atawasili Mahakamani muda wowote kuanzia sasa, na taarifa kamili ya kinachoendelea bado haijawekwa wazi.
