Hapa ndipo walipofikia Foby na Hamisa Mobetto

Jumamosi , 6th Jul , 2019

Msanii na mwandishi wa ngoma za Bongofleva Foby, amesema kwasasa wamemaliza tofauti kati yake na Hamisa Mobetto, ambaye ni mwanamitindo na mwimbaji pia.

Foby na Hamisa

Akiongea kwenye Friday Night Live ya East Africa, Foby ameweka wazi kuwa wametafutana kupitia mitandao ya kijamii na sasa wanawasiliana vizuri tu.

''Nadhani tulimisiana, alianza ku-like picha zangu Instagram na mimi nikafanya hivyo baadaye tukatafutana kwahiyo mambo yameisha tuko poa'', amefunguka Foby.

Foby na Hamisa walitofautiana baada ya Foby kuweka wazi kuwa mrembo huyo alimchinjia baharini baada ya kumuomba collabo ambayo yalikuwa ni makubaliano ya awali wakati anamwandikia ngoma yake ya kwanza ''Madam hero'.

Foby jana aliongozana na Pam D ambaye alikuja kutambulisha Video yake mpya inaitwa Kizunguzungu ambayo ilitoka Exclusive kwa mara ya kwanza kwenye FNL.