"Hata pesa imeshindwa kutugombanisha"-Oka Martin 

Ijumaa , 17th Jan , 2020

Wachekeshaji wawili wanaofanya vizuri mitandaoni, Oka Martin na Official Carpoza, wamesema hawajawahi kugombana kwenye maisha yao na urafiki wao hauwezi ukafa kwa sababu ya pesa au mapenzi.

Wachekeshaji Oka Martin upande wa kushoto,kulia ni Official Carpoza

Wakipiga stori na EATV & EA Radio Digital wameeleza kuwa, wao sio rahisi kugombana japokuwa huwa kuna kupishana kauli za hapa na pale ila wanawekana sawa maisha yanaendelea.

"Hatujawahi kugombana na sio rahisi na kingine hata pesa pia imeshindwa kutugombanisha, kwa sababu mimi ninaweza nikawa na pesa na yeye akalijua hilo, lakini naweza nikamuomba nizitumie pesa zake na bado akanipa" amesema Official Carpoza.

Aidha kwa upande wa Oka Martin ameongeza kusema "Huwa hatugombani ila tunapishanaga kauli  kwa sababu mmoja wetu anaweza akawa ameamka na mood mbaya ila uzuri ni kwamba tunafahamiana, kuna wakati ni kweli unakasirika na unashikwa na kitu ila tunaambiana tuache ujinga tunanuniana kwa sababu gani".

Pia wamesema walianza kuwa marafiki na wasanii wa muziki, kabla ya kuingia kufanya vichekecho ambavyo ndiyo vimewatambulisha zaidi kwa watu.