Jumatatu , 17th Feb , 2020

Msanii wa filamu na muziki Hemedy PHD, ni mmoja wa wasanii ambao wanajibu vibaya sana na kuwatukana mashabiki zake kwenye mitandao ya kijamii hususani wa Instagram.

Picha ya Hemedy PHD

Akiieleza EATV & EA Radio Digital, sababu za kuwatukana mashabiki zake msanii huyo amesema yeye sio mtu wa kuvumilia jambo ambalo litamgusa hisia zake, ndiyo maana atakaye-comment vibaya basi humrudishia na haogopi kushusha hadhi yake kisa kutukana watu.

"Kitu kimoja kuhusu mimi ni sijuagi kuvunga, kwahiyo kama unanigusa hisia zangu nafunguka kwa sababu ni mkweli, sio kama nasoma comment zote kwamba aliyesema vibaya nimjibu hapana, huwa nikifungua nikikuta comment mbaya ya juu basi huyohuyo ndiyo nitakayeshughulika naye"  amesema Hemedy PHD.