Jumatano , 11th Mar , 2015

Siku mbili tu zimebaki kuelekea Onyesho kubwa la mitindo na bidhaa za Harusi la Harusi Trade Fair kwa mwaka 2015, linatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 13 na jumamosi tarehe 14 mwezi huu, Danken House Mikocheni kuanzia saa mbili na nusu usiku.

Onyesho la mitindio na bidhaa za Harusi la Harusi Trade Fair 2015

Onyesho hilo litahusisha bidhaa za kipekee kabisa kutoka kwa wadau wakubwa na tiketi kwa ajili ya onyesho lenyewe zinaendelea kuuzwa pale Epidor Masaki kwa shilingi 25,000 kwa kawaida na 50,000 kwa VIP.

Hakikisha unashiriki ili kujipatia na pia kufahamu bidhaa bora na za kisasa kabisa kwa ajili ya shughuli yako ya Harusi.

Onyesho hili linaletwa kwako kwa udhamini wa nguvu kabisa wa East Africa Radio na East Africa Television.