Jay Z azamia katika bangi

Jumatano , 10th Jul , 2019

Mwana HipHop bilionea zaidi duniani Jay Z, sasa ameingia rasmi ubia na kampuni ya utengenezaji na uzalishaji wa biashara ya bangi iitwayo Caliva.

Msanii Jay Z

Jay Z amepewa nafasi ya mkurugenzi mkuu katika mipango mikakati ya kuiendeleza kampuni hiyo , na ameingia ubia huo wa kufanya nao kazi kwa mwaka mzima.

Katika nafasi hiyo Jay Z atakuwa anasaidia masuala ya ubunifu, maamuzi , juhudi za ufikiaji malengo na mikakati. Pia atakuwa ana dili na haki za kijamii kwenye mambo ya kuhahalilsha bangi, ikiwa pamoja na utetezi, mafunzo ya kazi, kuajiri wafanya kazi, na kufanya kazi kwa maendeleo.

"Nafanya kitu chochote, nataka nifanye kazi kwa usahihi katika ngazi za juu, uwezo wangu wote katika sekta hii ya biashara ya bangi, jitihada bora za kitaalamu katika ushiriki huu, tunataka kubuni kitu cha kushangaza, na kufanya vizuri ili kuleta watu katika njia" amesema Jay Z.

Jay Z sio mwana Hiphop wa kwanza kuingia kufanya biashara hii ya bangi wengineo ni Uncle Snoop Dogg, Wiz Khalifa, 2 Chainz Ty Dolla Sign na Ray J wote hawa na wana kampuni zao za utengenezaji na uzalishaji wa biashara ya bangi.